Mohammed Ali ni mtangazaji ambaye alijizolea umaarufu kutokana na kipindi chake cha Jicho pevu ambacho kiliwafungua wakenya wengi macho hususan kuhusu vitu vingi ambavyo wakenya hawangevijua.
Kilichobadilisha mkondo wake wa maisha ni baada ya yeye kujitosa katika kinyanganyiro cha kugombea ubunge katika eneo bunge la nyali.
Uchaguzi wa mchujo ulifanyika hivi majuzi na hakuibuka kuwa mshindi badala yake Abdalla ambaye ni nduguye Joho alishinda mchujo huo.
Hii ilidhirisha “unabii” ambao Kipchumba Murkomen alikuwa ametabiri hapo awali kuwa Mohammed Ali hawezi shinda uchaguzi wowote kenya