Thraw Back Thursday: Hivi C’zars Hitmaker wa Amka ukatike amewahi patikana? Pata habari kamili hapa

Alionekana mara ya mwisho mwaka wa
2006, na huo ndio wakati ambapo kapaji chake kilikuwa kimeiteka anga ya Afrika Mashariki. Amka ukatike ni wimbo wake wa kipekee alioufanya na uligusa zaidi. Kipaji chake kiligeuka fahari kubwa sana sio tu kwa wazazi wake Bali hata nchini Kenya.
Ni takriban zaidi ya miaka kumi na moja tangu aonekane na wengi wamejiuliza yuko wapi. Itakuwa vigumu kuruhusu akili kuamini kuwa C-zars yuko au anaishi sehemu fulani ya dunia. Ni binadamu gani anayeweza kujificha kwa zaidi ya miaka kumi na moja? Maswali ni mengi ambayo yataulizwa ila majibu hayapo.
Awali uvumi ulienea kuwa kilichomfanya apotee ni woga wa mtihani wa kitaifa, KCSE. Kunacho kipindi fulani habari ilijitokeza kuwa C’zars anaishi na mwanamke mzungu ambaye alimpa maisha ya kifahari japo uvumi huu haukuaminika.

Mtangazaji maarufu wa kipindi cha Mambo Mseto Mzazi Willy M Tuva, alijaribu kuihoji familia yake nayo familia ilidai kuwa haina habari yoyote kuhusu uwepo wa mwanao.
Wazazi wake wamejaribu kutoa pesa nyingi kwa yeyote atakayetoa habari yoyote kuhusu pahali alipo lakini bado mbinu hii haijafaulu.

Babake Abdul Karim Makasi
amekuwa na wakati mgumu hasa asijue ikiwa mwanawe yuko hai ama ameaga dunia. Ni uchungu sana kwa mzazi yeyote yule kukosa kumwona mtoto wake hususan wakati unashindwa kujua ikiwa yuko hai ama ama ameenda jongomeo. Maombi ya kila mtu ni kuwa siku moja C’zars atarudi nyumbani akiwa hai na furaha itarejea tena kwa familia ya mzee Makasi.