Picha: Huyu ndiye mchumba wake Harmonize

 

Harmonize ni mwanamziki anayekuwa kwa kasi nchini Tanzania. Mbali na kuwa uwepo wake kwenye wasafi record umechangia mafanikio yake, ukweli ni  kuwa Muimbaji Huyo ana kipaji kisichoelezeka.
Hivi maajuzi Wcb staa Harmonize alikuwa kwenye #FridayNiteLive na @sammisago akuongelea swala la mahusiano yake na Jackline Wolper na kusema ni mwanamke aliye mpenda sana.
Harmonize anasema “ Mwanamke mzuri kama Jackline sio wa kuficha na kukificha ni kama unahofia mtu mwingine asijue, Jack ananiweka powa,ananipunguzia mawazo ili nifanye nyimbo nzuri, niliahidi kwenye interview zangu wakati natoka kuwa nikipata mwanamke mwenye vigezo na nikaingia kwenye relationship lazima nitaweka wazi“.
Harmonize amekuwa kwenye stori nyingi za burudani kutokana na mahusiano yake na Jackline Wolper.