Msanii maarufu wa Bongo ameshtakiwa kwa Kosa linalohusu dawa za Kulevya

Aghalabu visa vya wasanii kukamatwa na dawa za kulevya huripotiwa kutoka bongo.

Ikubumbukwe kuwa hapo awali msanii TID, muigizaji Wema Sepetu na socialite maarufu Agnes Masogange waliwahifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la madawa za kulevya. Hii ni dhihirisho tosha kuwa swala la unga (dawa za kulevya), ni changamoto kubwa bongo.

Kisa cha hivi karibuni kinamhusu msanii Chidi Benz, ambaye alikamatwa pamoja na washukiwa saba wakiwa wanalangua unga. Kamanda Wa polisi eneo la Ilala Salum Hamduni, alithibitisha madai haya.

Chidi Benz amesaidiwa zaidi ya mara moja na wasanii wenzake ikiwemo Diamond Platnumz kwa kupelekwa REHAB, lakini inaonekana bado hajasoma wala kujifunza lolote.