Esther Akothee ni msanii anayependwa sana nchini kenya. Anaishi jijini mombasa ila asili yake ni kaunti ya kisumu.
Yeye ndiye msanii wa kipekee kutoka Kenya ambaye amepata fursa ya kushirikiana na msanii wa Tanzania Diamond platnumz kipenzi cha wengi.
Vile vile Akothee ameshirikiana na msanii mkali kutoka Nigeria Mr Flavour kitu ambacho kilimpa umaarufu zaidi sio tu bara la Afrika bali dunia nzima.
Anaaminika kuwa msanii mwenye utajiri mwingi zaidi nchini kenya. Japo wengi wanasema utajiri wake unatokana na “sponsor“, hit maker huyo wa benefactor amejitokeza aghalabu na kusema kuwa utajiri wake umetokana na namna amewekeza kwa bishara.