Hii ndio sababu Daniel Ndambuki maarufu kama Churchil amekashifiwa

Daniel Ndambuki maarufu kama Churchil ambaye pia anakiongoza kipindi cha churchil show amekashifiwa kwa kutowalipa vizuri wachekeshaji wanaomfanyia kazi.

Raptcha The scientist

Madai haya yalianzishwa Raptcha the scientist ambaye pia kipindi fulani alikuwa akichekesha katika kipindi cha churchil show.

Raptcha the scientist ambaye ni mtangazaji wa Hot 96 alionekana kufedheheshwa na namna mchekeshaji  Emmanuel Makori maarufu kama Ayeiya poa poa alipoaga dunia akiwa katika hali ya ufukara ilhali amekuwa akiwachekesha wakenya kwa kipindi kirefu.

Hata hivyo Raptcha aliwapa ushauri wachekeshaji wa churchil show kuwa wepesi wa kuwaza zaidi ili kutumia umaarufu wanaopata katika kipindi cha churchil show kujiimarisha kimaisha kama alivyofanya mchekeshaji Erick Omondi.

Hii hapa baadhi ya tweets alizozituma Raptcha The scientist