Anne Waiguru awaonyesha kivumbi wapinzani wake

Aliyekuwa katibu wa wizara ya ugatuzi na mipango ameonekana kushinda kura za mchujo katika kinyanganyiro kupitia chama cha Jubilee.

Kutoka kwa vituo 134 Waiguru alikuwa anaongoza kwa kura 33,890 huku akifuatwa  kwa ukaribu na mbunge wa kirinyaga ya kati Joseph Gitari akiwa na kura 14,909.

Cha kushangaza gavana wa sasa Joseph Ndathi  anachukua nafasi ya tatu akiwa na kura 6950.

Hata hivyo Kura zingali zinahesabiwa na huenda hata matokeo yakabadilika. Atakayeshinda kupitia Jubilee atachuana na wengine akiwemo kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua uchaguzi wa Agosti tarehe nane.